Programu huria ya software hutengenezwa na watu kama wewe. Jifunze jinsi ya kuzindua na kukuza mradi wako.
Ni Ijumaa! Wekeza saa chache kuchangia programu unayotumia na kupenda: opensourcefriday.com
Vidokezo vya kujitunza na kuepuka uchovu kama mtunzaji.
Je, ungependa kuchangia katika open source? Mwongozo wa kutoa michango ya open source, kwa wanaoanza na kwa maveterani.
Jifunze zaidi kuhusu ulimwengu wa Open Source na uwe tayari kuzindua mradi wako mwenyewe.
Saidia mradi wako wa open source kukua kwa kuufikisha kwa watumiaji wenye furaha.
Kujenga jamii inayohamasisha watu kutumia, kuchangia, na kuhubiri mradi wako.
Kufanya maisha yako kuwa rahisi kama mtunzaji wa open source, kutoka kwa kuandika nyaraka hadi kutumia jamii yako.
Kuendeleza miradi ya open source kunaweza kufaidika na sheria rasmi za kufanya maamuzi.
Dumisha kazi yako katika Open Source kwa kupata usaidizi wa kifedha kwa wakati wako au mradi wako.
Wezesha tabia ya jamii yenye afya na inayojenga kwa kupitisha na kutekeleza kanuni za maadili.
Fanya maamuzi yenye taarifa ili kusaidia mradi wako wa open source kufanikiwa kwa kupima na kufuatilia mafanikio yake.
Kila kitu ambacho umewahi kujiuliza kuhusu upande wa kisheria wa open source, na mambo machache ambayo hujui.